Bodi ya wakurugenzi ndani ya klabu ya Arsenal imeidhinisha mpango wa kocha wao wa kutumia kitita cha fedha ambacho kitaweka rekodi ya usajili nchini England lengo likiwa kumsajili mshambuliaji nyota wa klabu ya Real Madrid Karim Benzema.
Arsene Wenger kwa muda mrefu amekuwa akitamani kumsajili mchezaji huyu na bodi ya klabu hii imeidhinisha maombi ya kocha huyo ambapo sasa Arsenal iko tayari kufanya mazungumzo na Real Madrid kwa ajili ya mchezaji huyo.
Arsenal sasa iko tayari kupeleka ofa ya kati ya euro milioni 65 na 70 kwa ajili ya Benzema na hadi sasa hakuna klabu nyingine ambayo imefahamika kuwa na dhamira ya dhati kumsajili mshambuliaji huyo zaidi ya Arsenal.
Arsene Wenger amepewa fedha za kumsajili Karim Benzema wa Real Madrid.
Madrid huenda wakalazimika kumuuza mchezaji mmoja kwani wanataka kumsajili kipa wa Man United David De Gea na wanahitaji kuuza mchezaji ili kutengeneza fedha kwa ajili kipa huyo .
Post a Comment