photo Ad 728  x 90_zps6bmpgl6d.jpg
 

Unknown Unknown Author
Title: Rapper Jafarai kuja na ujio mpya
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Rapper Jaffarai anajipanga kuachia kazi mpya aliyomshirikisha Ommy Dimpoz ambayo amedai itakuwa na bajeti kubwa. Akizungumza , Jaffar...
Rapper Jaffarai anajipanga kuachia kazi mpya aliyomshirikisha Ommy Dimpoz ambayo amedai itakuwa na bajeti kubwa.

Akizungumza , Jaffarai amesema sababu iliyomfanya kuwekeza pesa nyingi kwenye kazi hiyo ni kuhitaji kupiga hatua kwenye muziki wake pamoja na video zake kuchezwa kwenye vituo vya nje.
“Wakati imenionyesha njia lakini pia muziki umebadilika sana. Sasa hivi kuna ngoma nimefanya na Ommy Dimpoz itabidi itoke na video kali,” amesema rapper huyo.
“Wimbo bila kufanya video kali naona kama wimbo hautafika mbali hivi. Mimi sitaki kutoa ngoma halafu iwe kawaida. Kuna ngoma nimefanya na Ommy Dimpoz hiyo ndo kazi mpya, inaitwa Maridadi, amefanya Man Watler. Hii ngoma inahitaji bajeti kubwa kama nilivyosema. Nataka ichezwe Trace TV na vituo vingine vikubwa. Nadhani mpaka budget ikikamilika ndio nitajua naanzia wapi lakini soon mashabiki wangu watapata kitu kizuri.”

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top