photo Ad 728  x 90_zps6bmpgl6d.jpg
 

Unknown Unknown Author
Title: Vanessa azungumzia collabo na Diamond, mipango na Jux, kama bado anafanya kazi na MTV Base na ukaribu na Alikiba
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Vanessa Mdee aliwekwa kwenye Kikaango cha EATV wiki hii ambapo mashabiki wake walipata fursa ya kumuuliza maswali mbalimbali yakiwemo ya uhu...
Vanessa Mdee aliwekwa kwenye Kikaango cha EATV wiki hii ambapo mashabiki wake walipata fursa ya kumuuliza maswali mbalimbali yakiwemo ya uhusiano wake na Jux na mipango yao ya baadaye.
11849143_129325920743371_2129688313_n
Akijibu swali la mipango aliyonayo na Jux, muimbaji huyo alisema wanatarajia furaha ya kudumu huku akidai kuwa hawana mpango wa kuwa na mtoto siku za hivi karibuni.
Pia Vanessa alidai kuwa amekuwa na uhusiano na Jux kwa mwaka mmoja na miezi minne sasa.
Kuhusu collabo na Diamond, Vee Money alisema itakuwepo muda si mrefu na anaamini kuwa itakuwa ya kuotea mbali.
Kuna mtu alimuuliza kama ana beef yoyote na Alikiba na Vanessa kujibu, “Ali Kiba sina beef naye infact sina beef na mtu yeyote. Nampenda nakumheshimu sana. Hatujawahi kufanya kazi ya mziki pamoja lakini ninamuamini sana ana kipaji sanaa na cha kipekee. Tunashirikiana kupinga ujangili kama mabalozi wa Wild Aid.”
Kuhusu kama bado anaendelea kufanya kazi na MTV Base, Vanessa alijibu, “Mdee Nimeacha kufanya vipindi vya kawaida nafanya vipindi maalum tu kama interview ya Neyo nilioifanya katika tuzo za MAMA 2015.”

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top