Hatimaye sakata la usajili wa kiungo mshambuliaji wa Kiargentina Angel Di Maria limefikia tamati muda mfupi uliopita.

Kupitia akaunti rasmi za mitandao ya kijamii ya vilabu vya Manchester United na PSG imethibitishwa rasmi Di Maria ameuzwa.
Di Maria, 27, juzi alifuzu vipimo vya afya alivyofanyiwa huko nchini Qatar – mjini Doha, nyumbani kwa wamiliki wa klabu hiyo.
Winga huyo anategemewa kutambulishwa rasmi leo jioni huko Paria Ufaransa na atasaini mkataba wa miaka minne kuitumikia PSG.

Di Maria aliyenunuliwa kwa ada ya uhamisho wa £59.7m, anaripotiwa kuuzwa kwenda PSG kwa ada ya £44m mwaka mmoja baada ya kujiunga na United.
Post a Comment