
Nimekutana na interview moja aliyofanya kaka yake Tupac Shakur, Mapreme Shakur siku chache zilizopita na mmoja ya vitu alivyoulizwa kwenye interview hiyo ni kama ni kweli Janet Jackson alikataa kufanya scene ndogo ya mapenzi na 2Pac mwaka 1992 mpaka apime UKIMWI...
Kwenye interview Mopreme Shakur aliulizwa >>> “Nilisikia
stori moja kuhusu movie ya 2Pac ya Poetic Justice kuwa Janet Jackson
alikataa kufanya scene ya mapenzi na 2Pac mpaka apime UKIMWI kitu kama
hicho?<<< Mopreme alijibu hivi..

Tupac Shakur na Janet Jackson kwenye movie ya Poetic Justice (1992).
>>>“haha
haikuwa scene ya mapenzi ilikuwa scene ndogo ya Janet kumpatia kiss
2Pac, na siku chache kabla ya siku ile Janet alikuwa ametoka kushoot
movie nyingine alafu akaumwa mafua…sio kwamba aliyekuwa nae
alimuambukiza lakini ilitokea tu alipata mafua…sasa akamwambia 2Pac ooh
unajua itabidi ukapime UKIMWI kwanza ndio tukiss sio kwa ubaya
lakini…2Pac hakuelewa kabisa..hakuelewa!”<<< Mopreme Shakur.

Poetic Justice (1992).
>>>“alisema
kama nitakuwa nae kimapenzi baada ya hapa basi sawa nitapima UKIMWI
lakini kwa kitu kidogo kama hiki nikapime UKIMWI kwanini!? 2Pac
hakupenda ile kauli kabisa…ilikuwa tabu ila badaae waliyamaliza..so yeah
ilishawahi kutokea.”<<< Mopreme Shakur.
Hapa chini nimekusogezea sauti ya Mopreme Shakur akielezea jinsi ilivyokuwa kipindi hicho kati ya Janet Jackson na kaka yake.
Post a Comment