
Msanii wa Hiphop Marekani mwenye style yake ya kipekee kabisa ya ku-rap Busta Rhymes anaziandika headlines kwenye kurasa za burudani.
Siku chache zilizopita msanii huyu alikuwa Gym moja iitwayo Steel Gym maeneo ya Chelsea jijini New York na wakati akiwa mazoezini msanii huyo aliingia kwenye majibishano na mtu mwengine kwenye Gym hiyo.

Mabishano yakasababisha ugomvi mkubwa kati ya wawili hao, Busta Rhymes akapandwa
na hasira na kumrushia mwenzake chupa…mwanaume huyo alieumia alikataa
kupewa huduma ya kwanza na Gym hiyo bali akaamua kwenda moja kwa moja
kwenye kituo cha polisi na kufungua mashitaka ya ushambuliaji dhidi ya Busta Rhymes.

Mwanasheria wa Busta Rhymes
amesema kitendo hicho ni cha kijinga kwani ugomvi aliuanzisha yeye na
sio Busta kitendo cha kumshitaki ni nia mbaya ya kulichafua jina la
msanii huyo… kwa sasa Busta Rhymes anashikiliwa na kituo cha polisi kwa mashitaka hayo.
Post a Comment