photo Ad 728  x 90_zps6bmpgl6d.jpg
 

Unknown Unknown Author
Title: Mahakama yamuachia Rick Ross kwa dhamana ya dola milioni 2 za kimarekani.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Headlines za Entertainment Marekani zilikuwa na story ya Rick Ross kukamatwa na kuwekwa ndani yeye pamoja na bodyguard wake, kesi yao i...
Rick-Ross-court
Headlines za Entertainment Marekani zilikuwa na story ya Rick Ross kukamatwa na kuwekwa ndani yeye pamoja na bodyguard wake, kesi yao ilikuwa ni ishu ya kuteka na kujeruhi watu wawili.
July 01 2015 kapandishwa Mahakamani, Georgia Marekani.. Kesi ikasomwa na milango ikawa wazi kwa jamaa kuwekewa dhamana.
Rick-Ross-Fed-Up-With-Jail-Lawyer-Argues-For-Bail-In-Court
Yuko Uraiani baada ya Mahakama kukubali dhamana ya dola Milioni 2 (ni zaidi ya Bilioni 4 Tshs), na sio hiyo pekeake.. kuna masharti ambayo Mahakama imempa pia, ikitokea akaingia mtaani alafu akavuruga tena basi atakuwa amelipoteza Jumba lake lenye thamani ya zaidi ya Bilioni 5 !!
Rick hajaachiwa hivihivi mtu wangu, Mahakama imeamrisha jamaa afungwe kifaa ambacho kinaitwa GPS Monitor mguuni, kokote anakopita wao watakuwa wanamfuatilia.
Hiki ni kipande cha video ya kwanza toka Mahakamani, hapa mashitaka yanasomwa.

Hiki ni kipande cha video ya pili.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top